Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026 imetoa tuzo za shukrani kwa viongozi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Jeshi la Polisi, kama kutambua mchango wao katika kudumisha amani, mshikamano na ushirikiano wa kijamii.
Tuzo hizo zilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Mheshimiwa Leila Bhanji, ambaye aliambatana na viongozi wa Jumuiya ya Madhehebu ya Kiislamu Tanzania (JMAT) Kanda ya Ziwa, wakiongozwa na Mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Mwanza.

Katika hafla hiyo, tuzo zilikabidhiwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Saidi Mohamed Mtanda, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Wilford Mutafungwa.
Aidha, viongozi hao walitembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, ambapo walipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Omary Mtuwa.
Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026 imepongezwa kwa juhudi zake kubwa katika maandalizi ya tukio hili muhimu na lenye heshima, linalolenga kuimarisha umoja, amani na mshikamano katika jamii.
Your Comment